8 Juni 2015 - 11:35
Umoja wa Ulaya waitaka Iran kukubali kuchunguzwa vituo vyake vya kijeshi

Shirika la kudhibiti silaha za kinyuklia la umoja wa Mataifa IAEA linakabiliwa na kesi ya kuvujisha siri za nyuklia za Iran, ambazo hazikutakiwa zivuje, kuvuja kwa siri hizo kulipelekea wataalam watatu nyukia wa Iran kuuawa

Umoja wa Ulaya unaitaka Iran kutoa ushirikiano katika kufanyiwa uchunguzi na Umoja wa Mataifa kuhusiana na madai kuwa ilitaka kuunda silaha za kinyuklia iwapo inataka makubaliano kamili kati yake na nchi sita zenye nguvu zaidi duniani kufikiwa ambayo yatapelekea kuondolewa vikwazo dhidi yake. Taarifa hiyo ya Umoja wa Ulaya iliyotolewa leo inakuja huku Iran na nchi wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa Matifa pamoja na Ujerumani zikitarajiwa kufikia makubalinao tarehe 30 mwezi huu. Shirika la kudhibiti silaha za kinyuklia la umoja wa Mataifa IAEA linafanya mkutano hii leo. Iran imekanusha kuwa ilijaribu kuunda silaha hizo za kinyuklia au kuwa na nia ya kufanya hivyo na imekataa kushirikiana na IAEA kuchunguzwa katika kambi zake na vituo vya kijeshi. Umoja wa Ulaya umesema uchunguzi wa kina kuhusu madai hayo utakuwa muhimu kufikia makubaliano.

Shirika la kudhibiti silaha za kinyuklia la umoja wa Mataifa IAEA linakabiliwa na kesi ya kuvujisha siri za nyuklia za Iran, ambazo hazikutakiwa zivuje, kuvuja kwa siri hizo kulipelekea wataalam watatu nyukia wa Iran kuuawa, Shirika la kudhibiti silaha za kinyuklia la umoja wa Mataifa IAEA liliishia tu kuomba msamaha kwa makosa iliyofanya.

Kwasasa serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran inapinga vikali kuchunguzwa vituo vyake vya kijeshi na pia inapinga vikali kuwaweka hadharani wataalam wake wa nyuklia.

Jamhuri ya kiislam ya Iran imetoa sharti kwamba makubaliano yatafikiwa pale tu yatakapokuwa ni makubaliano yanayokubalika kisheria na kiakili.

Serikali ya Iran imeendelea kusisitiza kwamba kutofikia makubalino ni bora kwa nchi yake kuliko kufikia makubaliano yasiyo na vigezo vya kimantiki.